Tel: +254 (0)20 2271000/ 20

Email: ashc@cabi.org

Plantwise

Mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao

Summary:

Mwongozo huu una lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri mazao muhimu ya chakula yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, nini cha kufanya ili kuzuia kutokea na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea. Chaguzi za usimamizi wa kila mdudu au ugonjwa zimegawanywa katika ‘mbinu za kitamaduni’, kama vile matumizi ya aina sugu, mbegu safi, kilimo cha mzunguko na hali nzuri ya usafi shambani, na ‘mbinu za kikemikali’, ambazo huhusisha matumizi ya dawa sahihi za kuua wadudu. Aidha maelezo yanatolewa juu ya viumbe vinavyosababisha tatizo na madhara yake. Hatimaye, orodha fupi ya machapisho na tovuti inatolewa ambapo maelezo ya ziada yanaweza kupatikana.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015. Mazao yaliyoangaziwa ni: nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 2.6 MB)

Wadudu na magonjwa ya mazao Mizizi – Kiswahili

Summary:

Kadi hizi zina lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri mizizi yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika. Zimetolewa kwa mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao, yakiangazia mazao kama nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 3.7 MB)

Wadudu na magonjwa ya mazao mikunde Swahili

Summary:

Kadi hizi zina lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri mikunde yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika. Zimetolewa kwa mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao, yakiangazia mazao kama nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 3.1 MB)

Wadudu na magonjwa ya mazao nafaka – Swahili

Summary:

Kadi hizi zina lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri nafaka yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika. Zimetolewa kwa mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao, yakiangazia mazao kama nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 3.7 MB)

Wadudu na magonjwa ya mazao – Migomba

Summary:

Kadi hizi zina lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri migomba yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika. Zimetolewa kwa mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao, yakiangazia mazao kama nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015.

 

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 1.8 MB)

Pest factsheet: Yam dry rot

Summary:

This guide sets out the causes, impact, signs and symptoms of yam dry rot and offers practical advice on management through prevention and control strategies.

Languages:
English
Read More Download (.pdf 354.8 KB)

Ugonjwa wa mabaka ya shina na shina la jani wa viazi tamu – Alternaria bataticola

Summary:

MUHTASARI: Ugonjwa wa shina na shina la jani wa viazi tamu (pia uitwao Alternaria blight ya
viazi tamu), husababishwa na kuvu Alternaria bataticola. Hutokeza kama madoa juu ya majani, shina la jani, na mashina, na kusababisha majani kuanguka na mashina kufa. Hupatikana katika nchi kadhaa za Afrika lakini ni mbaya zaidi hasa katika mazingira ya baridi na unyevu ya Kati na Kusini Magharibi mwa Uganda. Usimamizi ni kupitia matumizi ya aina za viazi zilizochaguliwa au kuzalishwa ili ziwe na usugu au uvumilivu, kuchagua vipanzi kwa makini na kudumisha usafi, hasa uharibifu wa mashina baada ya kuvuna.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 1.2 MB)

Dieback ya viazi vikuu Colletotrichum gloeosporiodies

Summary:

MUHTASARI: Ugonjwa wa dieback ya viazi vikuu (Dioscorea alata), pia unaojulikana kama anthracnose ya viazi vikuu maji, husababishwa na kuvu Colletotrichum gloeosporioides. Husababisha madoa meusi kwenye majani, kuanguka kwa majani, na kufa kwa chipukizi changa na kupungua mazao ya viazi. Maambukizi huanza kama mbegu za kuvu kutoka kwa mimea mingine, kwekwe na viazi vilivyoambukizwa. Huenea kupitia upepo na mvua, na viazi vyenye ugonjwa. Ugonjwa hudhibitiwa kwa kutumia aina zinazohimili ugonjwa na kwa kupanda mapema, kabla ya msimu wa mvua nzito.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 499.7 KB)

Nondo wa viazi vikuu

Summary:

MUHTASARI: Viwavi wa aina mbalimbali za nondo ni wadudu waharibifu wa viazi vikuu baada ya mavuno barani Afrika. Kusafisha ghala na kutohifadhi viazi vilivyoharibika hupunguza uharibifu. Pia kuna dawa za misingi ya miti na za kuunda zinazoweza kutumika kwa viazi vikuu vilivyohifadhiwa ili kudhibiti mayai, viwavi na nondo waliokomaa.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 99.5 KB)

Fukusi wa maharage – Acanthoscelides obtectus

Summary:

MUHTASARI: Fukusi wa maharage ni mdudu mharibifu mkubwa wa aina nyingi za maharage baada ya kuvuna. Mashambulizi huanza shambani, lakini linakuwa tatizo kubwa baada ya mavuno kwa kuwa matundu yaliyoachwa kwenye maharagwe hupunguza thamani ya mazao. Ili kuzuia mashambulizi makubwa, ni muhimu kuvuna maharagwe haraka mara tu yanapokomaa. Kuweka maharage katika hifadhi safi ni hatua muhimu zaidi. Ondoa maharagwe ya zamani kutoka kwa ghala na utumie dawa kusafisha ghala kama ni lazima. Tumia chombo cha kuhifadhi ambacho hakiingizi hewa kama inawezekana.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 399.8 KB)