Tel: +254 (0)20 2271000/ 20

Email: ashc@cabi.org

Yam

OFRA Book on Fertilizer Use Optimization in Sub-Saharan Africa

Summary:

Fertilizer Use Optimization in Sub-Saharan Africa is a 228 page book that provides a detailed explanation on optimizing fertilizer use within an Integrated Soil Fertility Management Framework in 13 African countries. The book is an output of the Optimizing Fertilizer Recommendations in Africa (OFRA) project, funded by AGRA.

Languages:
English
Read More Download (.pdf 13 MB)

Mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao

Summary:

Mwongozo huu una lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri mazao muhimu ya chakula yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, nini cha kufanya ili kuzuia kutokea na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea. Chaguzi za usimamizi wa kila mdudu au ugonjwa zimegawanywa katika ‘mbinu za kitamaduni’, kama vile matumizi ya aina sugu, mbegu safi, kilimo cha mzunguko na hali nzuri ya usafi shambani, na ‘mbinu za kikemikali’, ambazo huhusisha matumizi ya dawa sahihi za kuua wadudu. Aidha maelezo yanatolewa juu ya viumbe vinavyosababisha tatizo na madhara yake. Hatimaye, orodha fupi ya machapisho na tovuti inatolewa ambapo maelezo ya ziada yanaweza kupatikana.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015. Mazao yaliyoangaziwa ni: nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 2.6 MB)

Wadudu na magonjwa ya mazao Mizizi – Kiswahili

Summary:

Kadi hizi zina lengo la kutoa habari wazi zinazowezesha kuchukua hatua juu ya wadudu na magonjwa muhimu zaidi yanayoathiri mizizi yanayokuzwa na wakulima wadogo barani Afrika. Zimetolewa kwa mwongozo wa wadudu na magonjwa ya mazao, yakiangazia mazao kama nafaka (mahindi, mawele, mtama, mpunga), mikunde (njugu, maharagwe na kunde) mazao ya mizizi (mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu) na migomba.

Kwa kila mdudu au ugonjwa, maelezo yanatolewa ya jinsi ya kutambua tatizo, na jinsi ya kudhibiti wakati linapotokea.

Timu ya wataalam wa afya ya mimea wamekusanya maelezo haya; kwa kufanya hivyo wametumia utafiti na taarifa za hivi karibuni zinazopatikana mwaka wa 2015.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 3.7 MB)

Pest factsheet: Yam dry rot

Summary:

This guide sets out the causes, impact, signs and symptoms of yam dry rot and offers practical advice on management through prevention and control strategies.

Languages:
English
Read More Download (.pdf 354.8 KB)

Dieback ya viazi vikuu Colletotrichum gloeosporiodies

Summary:

MUHTASARI: Ugonjwa wa dieback ya viazi vikuu (Dioscorea alata), pia unaojulikana kama anthracnose ya viazi vikuu maji, husababishwa na kuvu Colletotrichum gloeosporioides. Husababisha madoa meusi kwenye majani, kuanguka kwa majani, na kufa kwa chipukizi changa na kupungua mazao ya viazi. Maambukizi huanza kama mbegu za kuvu kutoka kwa mimea mingine, kwekwe na viazi vilivyoambukizwa. Huenea kupitia upepo na mvua, na viazi vyenye ugonjwa. Ugonjwa hudhibitiwa kwa kutumia aina zinazohimili ugonjwa na kwa kupanda mapema, kabla ya msimu wa mvua nzito.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 499.7 KB)

Nondo wa viazi vikuu

Summary:

MUHTASARI: Viwavi wa aina mbalimbali za nondo ni wadudu waharibifu wa viazi vikuu baada ya mavuno barani Afrika. Kusafisha ghala na kutohifadhi viazi vilivyoharibika hupunguza uharibifu. Pia kuna dawa za misingi ya miti na za kuunda zinazoweza kutumika kwa viazi vikuu vilivyohifadhiwa ili kudhibiti mayai, viwavi na nondo waliokomaa.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 99.5 KB)

Mende mkubwa na mdogo wa viazi vikuu

Summary:

MUHTASARI: Mende mkubwa na mdogo wa viazi vikuu (Greater na lesser yam beetle) ni wadudu muhimu waharibifu wa viazi vikuu Afrika Magharibi. Mende aliyekomaa huchimba mchangani na kula viazi. Njia za kuzuia, kama vile kupanda mwisho wa msimu na kujaribu kuchelewa iwezekanavyo; na, kutibu mbegu za kupandia na dawa ya wadudu kabla ya kupanda, ni njia bora za kudhibiti mende wa viazi vikuu ili upunguze uharibifu wao.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 443.6 KB)

Ugonjwa wa batobato la viazi vikuu

Summary:

MUHTASARI: Kuna virusi angalau aina nne vinavyoambukiza viazi vikuu vya chakula katika Afrika Magharibi, ambapo virusi vya batobato la viazi vikuu ni muhimu sana katika usambazaji, matukio na athari juu ya ukuaji wa mimea. Mimea iliyoathiriwa huonyesha mabato, uharibifu, na katika hali kali, majani huwa kama kamba, ukuaji mbaya na mizizi midogo kuliko ile ya mimea yenye afya nzuri. Husambazwa kupitia viazi vinavyotumika kwa upanzi na vidukari. Mbinu muhimu zaidi za usimamizi ni matumizi ya aina mpya kutoka kwa mpango wa uzalishaji, kudhibiti kwekwe na uteuzi mashambani wa mimea yenye afya kama ‘mbegu’.

Languages:
Swahili / Kiswahili
Read More Download (.pdf 230.5 KB)

Muozo mkavu wa viazi vikuu

Summary:

Mwongozo huu unaweka sababu, athari, ishara na dalili za muozo mkavu wa viazi vikuu na unatoa ushauri wa vitendo juu ya usimamizi kupitia mikakati ya kinga na udhibiti.

Languages:
English
Read More Download (.pdf 380.6 KB)

Roots and tuber crop pests and diseases – summary cards

Summary:

These summary cards have information on the most important pests and diseases affecting roots and tubers by smallholder farmers in Africa. They are based on the crop pests and diseases manual covering crops such as cereals (maize, millet, sorghum, rice), legumes (groundnuts, beans and cowpeas) roots and tubers (cassava, sweet potato, yam) and banana.

For each pest or disease, information is provided on how to recognise the problem and manage it.

A team of plant health experts has compiled this information; in doing so they have drawn upon the latest research and information available in 2015.

 

Languages:
English
Read More Download (.pdf 439.3 KB)